27 Desemba 2025 - 14:38
Hitaji kuu la dunia leo ni mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu / Shambulio la Marekani lilishindwa mbele ya ujasiri wa vijana wa Iran

Ayatollah Khamenei, katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 59 wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya, amesisitiza kuwa sababu kuu ya msukosuko na wasiwasi wa madhalimu wafisadi si suala la nyuklia, bali ni kuinuliwa kwa bendera ya kupinga mfumo usio wa haki na utawala wa mabavu wa mfumo wa ubeberu duniani, pamoja na mwelekeo wa Iran ya Kiislamu kuelekea kujenga mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Ayatollah Khamenei, katika ujumbe wake kwa Mkutano wa 59 wa Mwaka wa Umoja wa Vyama vya Wanafunzi wa Kiislamu barani Ulaya, akirejea kushindwa kwa mashambulizi makubwa ya kijeshi ya jeshi la Marekani pamoja na kiongezo chake cha aibu katika eneo hili kutokana na ubunifu, ujasiri na kujitolea kwa vijana wa Iran ya Kiislamu, amesisitiza kwamba: sababu kuu ya msukosuko wa madhalimu wafisadi si mjadala wa nyuklia, bali ni kuinuliwa kwa bendera ya kupinga mfumo usio wa haki na mabavu ya mfumo wa ubeberu duniani, na kuelekea kwa mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu kwa upande wa Iran ya Kiislamu.

Matini / Andiko kamili la ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kama ifuatavyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu

Vijana wapendwa!

Mwaka huu nchi yenu, kwa baraka ya imani, umoja na kujiamini, imepata hadhi na uzito mpya duniani. Mashambulizi makubwa ya jeshi la Marekani na kiongezo chake cha aibu katika eneo hili yalishindwa mbele ya ubunifu, ujasiri na kujitolea kwa vijana wa Iran ya Kiislamu. Imethibitika kuwa taifa la Iran, kwa kutumia uwezo wake wenyewe, chini ya kivuli cha imani na matendo mema, na katika kukabiliana na madhalimu wafisadi na waonevu, linaweza kusimama imara na kuifikishia dunia mwito wa thamani za Kiislamu kwa sauti iliyo kubwa zaidi kuliko wakati wowote ule.

Huzuni kubwa kutokana na kuuawa shahidi kwa idadi ya wanazuoni, makamanda na baadhi ya wananchi wetu wapendwa haijaweza, wala haitaweza, kuwazuia vijana wa Iran wenye azma. Familia za mashahidi hao zenyewe ziko miongoni mwa viongozi wa mstari wa mbele wa harakati hii.

Suala si mjadala wa nyuklia wala mambo mengine ya aina hiyo. Suala ni kupambana na mfumo usio wa haki na utawala wa mabavu wa mfumo wa ubeberu katika dunia ya leo, na kuelekea katika mfumo wa haki wa kitaifa na kimataifa wa Kiislamu. Hili ndilo dai kubwa ambalo Iran ya Kiislamu imeinua bendera yake na kuwafanya madhalimu wafisadi na waharibifu kuwa na wasiwasi na ghadhabu.

Ninyi wanafunzi, hasa mlio nje ya nchi, mna sehemu ya jukumu hili kubwa juu ya mabega yenu. Zikabidhini nyoyo zenu kwa Mwenyezi Mungu, zitambueni uwezo wenu, na ziepusheni jumuiya zenu katika mwelekeo huu.

Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, na ushindi kamili unawasubiri, Insha’Allah.

Sayyid Ali Khamenei

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha